Salaam,
Ninayo furaha kubwa kukualika katika hafla maalum ya uzinduzi wa tovuti yetu mpya ya shirikisho la wanafunzi (TASAFIC WEBSITE). Uzinduzi huu utafungua mlango wa teknolojia mpya na huduma bora ambazo zimebuniwa kwa ajili ya kurahisisha na kuboresha mawasiliano kwa wanafunzi na kwa watu watu wengine. Hafla hii itafanyika kama ifuatavyo: Tarehe 8/6/2024 Muda: 10:00 jioni kwa saa za Beijing.Mahali: Oline meeting itafanyika katika mtandao wa Tencent wa namba (Meeting ID: 947-757-995).
Kutakuwa na maonyesho ya moja kwa moja ya vipengele na uwezo wa tovuti mpya, hotuba fupi kutoka kwa Mh. Khamis Musa Omar Balozi wa Tanzania nchini China.
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa kujibu barua pepe hii au kwa kuwasiliana nasi kupitia simu nambari +8613021205910 kabla ya Tarehe 6/6/2024.
Asante kwa kuwa sehemu ya safari yetu. Ushiriki wako ni wa thamani kubwa kwetu na tunajua utafurahia kile ambacho tumeandaa.
Kwa heshima,
Amosi L.P.Mbuji
Mwenyekiti-TASAFIC 2023/2024